Jump to content

2026:Ufadhili

From Wikimania
This page is a translated version of the page 2026:Scholarships and the translation is 92% complete.
Outdated translations are marked like this.


Under review

Ufadhili wa Wikimania 2026 sasa umefunguliwa!

Maombi [$1 sasa yanapokelewa]. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu mchakato mzima kwenye ukurasa huu. Ikiwa una changamoto, tafadhali wasiliana na $2

Ufadhili wa Wikimania ni nini?

Ufadhili ni ruzuku inayotolewa kwa mtu binafsi ili kumwezesha kuhudhuria Wikimania 2026 kwa ushiriki wa ana kwa ana. Wapokeaji wa ufadhili huchaguliwa na Kamati ya Ufadhili ya Timu Kuu ya Waandaaji wa Wikimania 2026, na fedha hutolewa na Wikimedia Foundation.

Ufadhili unajumuisha gharama za ndege, malazi, usajili, na posho ya kila siku kwa ajili ya mahitaji madogo na chakula wakati wa siku za mkutano wa awali na mkutano wenyewe, pamoja na bima ndogo ya afya. Kulingana na awamu ya mwanzo ya uthibitisho wa ufadhili, huenda kukapatikana idadi ndogo ya ufadhili wa sehemu ya gharama.

Fomu ya kuomba [ Done Ufadhili wa Usafiri wa Wikimania] kwa ajili ya Wikimania 2026 itakuwa wazi kuanzia tarehe 10 Septemba hadi Ijumaa, tarehe 31 Oktoba 2025.

Nani anaweza kuomba?

Kama ilivyokuwa awali, yeyote anayeweza kuthibitisha mchango wake au shughuli katika Wikimedia anakaribishwa kuwasilisha maombi. Mifano ni kama ifuatavyo:

  • Ushiriki hai (zaidi ya kuwa mwanachama na kutimiza wajibu wa uanachama pekee) katika aina fulani ya kikundi au shirika la Wikimedia (committee, hub, chapter, thematic organization, au user group).
  • Kushiriki katika matukio yaliyoandaliwa na Wikimedia (mfano, wapiga picha wanaochangia kwenye Wiki Loves Monuments, au washiriki wa warsha).
  • Kushiriki katika programu ya Wikimedia (mfano, ushirikiano wa GLAM au programu za elimu).
  • Kuandaa matukio au mashindano ya Wikimedia (mfano, Wiki Loves Monuments, au hafla za kuhariri makala – edit-a-thons).
  • Kuwa steward, CheckUser, mwanachama wa VRT, mkabidhi wa kiolesura, mkabidhi(admin), au mwenye haki nyingine za ziada (wa sasa au wa zamani).
  • Kuwa mpokeaji wa ruzuku wa Wikimedia Foundation.
  • Mchango katika msimbo wa MediaWiki, uundaji wa vifaa vidogo (gadgets) au zana nyingine kwa ajili ya miradi ya Wikimedia.

Hiyo ni mifano tu, hata hivyo. Nenda kwenye sehemu ya Ushauri wa Kina, soma mapendekezo yaliyo kwenye jedwali, kisha fikiria jinsi utakavyojibu maswali hayo kwa ‘njia yako’.

Kama una maswali, nenda kwenye sehemu ya ‘Nani anaweza kuomba’ katika Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ). Ikiwa bado una maswali zaidi, unaweza kutuma barua pepe kwa wikimania-scholarships@wikimedia.org.

Mchakato wa Ufadhili wa Wikimania ni upi?

Kwa ujumla, tunatarajia mchakato wa maamuzi ya ufadhili ufanyike kupitia hatua zifuatazo:

  1. Watu binafsi wanawasilisha fomu za maombi kupitia LimeSurvey.
  2. Watu binafsi wataona skrini ya uthibitisho na wataelekezwa jinsi ya kuhifadhi maombi yao kama PDF ikiwa watataka.
  3. Kikundi kinachoshughulika na Ufadhili kinachunguza uhalali wa maombi.
  4. Kikundi kinachoshughulika na Ufadhili kinakikisha maombi na kufanya maamuzi. Pia tutatekeleza mchakato wa Trust & Safety ili kuthibitisha uhalali wako katika hatua za baadae za mchakato.
  5. Watu binafsi wanajulishwa juu ya maamuzi na wanaombwa kutoa taarifa binafsi ili Wikimedia Foundation iweze kupanga usafiri na malazi.
  6. Wikimedia Foundation inapanga na kuthibitisha usafiri na malazi.

Vikao vijavyo vya utangulizi

Timu Kuu ya Waandaaji imeendesha vikao wa wazi kwa kila mtu anayevutiwa kuomba ufadhili wa Wikimania 2026. Vikao vilifanyika kwa lugha nne rasmi za tukio: Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa, na Kihispania. Tafadhali pata matoleo yaliyorushwa (recorded) hapa chini.

Ajenda

  • Utangulizi wa Wikimania 2026
  • Muhtasari wa mchakato wa maombi na uchaguzi wa ufadhili
  • Mubashara Q&A

Ushauri wa kujaza fomu ya maombi

Ushauri wa kina

  • Kujaza fomu ya maombi kutachukua takribani dakika 45–60. Huwezi kuhariri maombi baada ya kuyatuma. Unaweza kuya hariri kabla ya kutuma tu ikiwa hujafuta vidakuzi. Tunapendekeza ufanye kazi ya maombi yako kwenye hati tofauti kisha uikopie/kubandika majibu yako pale utakapo kuwa tayari, ili kuepuka hatari yoyote ya kupoteza kazi yako. Tafadhali usitume maombi mara mbili.
  • Kwenye ukurasa wa mwisho wa fomu ya maombi, utaona chaguo la kuchapisha maombi yako. Chaguo hili litakuongoza kuhamisha maombi kuwa kwenye muundo wa PDF kwa ajili ya kuhifadhi nakala yako binafsi — iwapo itahitajika tu.
  • Unaweza kuwasilisha maombi yako kwa lugha yoyote zinazotumika Wikimania 2026 – Kiarabu, Kifaransa, Kiingereza, au Kihispania. Ikiwezekana, tafadhali zingatia kuwasilisha katika moja ya lugha hizi kwani ndizo zinazozungumzwa na wanachama wote wa timu inachoshughulika na ufadhili. Pia, zingatia kuwa utahitaji kiwango cha kutosha cha Kiingereza kwa kushiriki na kujitolea katika tukio hilo bila shaka.
  • Tunaomba kwa unyenyekevu ueleze kwa uwazi mchango wako binafsi katika juhudi za kikundi. Hatukubali mafanikio ambayo hayawezi kuthibitishwa au yanayodaiwa uliyoyafanya wewe peke yako kwa uongo, ikiwa kwa ukweli yalikuwa juhudi za kikundi. Ongeza kiunganisho cha Diff, ukurasa wa wiki, au hata chapisho kwenye mitandao ya kijamii kitakachotusaidia kuthibitisha kama kweli umefanya kile unachodai kuwa ni chako.
Swali Kidokezo
Maelezo ya usafiri na mawasiliano Katika sehemu hii tafadhali kuwa sahihi na majibu yako. Maswali zaidi kuhusu taarifa ndani ya pasipoti yako n.k. yataombwa ikiwa tu wewe ni mpokeaji aliyefaulu.
Takwimu za demografia Tunaomba taarifa hizi kwa ajili ya takwimu, ili kuhakikisha kwamba utofauti wa maombi unaakisiwa katika utoaji wa ufadhili. Kujibu maswali haya ni hiari kabisa. Taarifa hizi zitachapishwa tu kwa muhtasari wa jumla.
Maswali ya tathmini Maswali yafuatayo ni maswali ya msingi ambayo maombi yako yatatathminiwa.

Tuna hamu ya kusoma maoni mazuri yenye viungo vya uthibitisho

Mada ya Wikimania 2026 ni ‘Uhuru, Usawa, Uaminifu.’ Hii inamaanisha nini kwako? Tunatafuta majibu ya ubunifu na yenye ufahamu kuhusu jinsi mada hii inavyolingana na michango yako katika Wikimedia. Je, kazi yako imechangia vipi katika kusaidia “Uhuru, Usawa, na Uaminifu” ndani ya harakati yetu? Tunapendekeza jibu la aya moja. Tafadhali thibitisha marejeleo yoyote ya kazi yako mwenyewe kwa viungo pale inapowezekana.
Ikiwa mtu angekuuliza, "Wewe au jumuiya yako ya ndani imefanya nini katika harakati za Wikimedia", ungejibuje? Kama wewe ni mpya katika harakati za Wikimedia, ni nini kilikushawishi kujiunga na jamii yetu? Tunataka kuelewa jinsi unavyoelezea ushiriki wako katika Wikimedia kwa watu walioko ndani ya harakati hii, na pia kwa wale ambao huenda hawana uelewa mkubwa kuhusu harakati au jamii yako. Michango yako imeleta athari gani? Umeshirikianaje na jamii yako kuendeleza dhamira yetu ya maarifa huru? Kwa washiriki wapya ambao huenda bado hawana mengi ya kushirikisha kuhusu athari zao, tungependa kuelewa jinsi ulivyofika hapa na kile unachotarajia kupata na kuchangia ndani ya harakati yetu. Tunapendekeza jibu la aya moja. Tafadhali thibitisha marejeleo yoyote ya kazi yako mwenyewe kwa viungo pale inapowezekana.
Tuambie kuhusu ushiriki wako wa hivi karibuni katika wiki yako ya nyumbani au katika harakati za Wikimedia kwa ujumla. Ni nini umejenga au umechangia ili kuboresha wiki yako au jamii yako? Je, umeongoza au kuandaa mojawapo ya shughuli hizi? Ni shughuli gani iliyokuwa na umuhimu mkubwa zaidi kwako binafsi, bila kujali matokeo yake?  Kwa swali hili, tunazingatia zaidi ushiriki na shughuli za miezi 18 iliyopita, kwa hivyo tafadhali hakikisha unazieleza kwa makusudi. Ikiwa ni lazima, unaweza pia kutaja shughuli za muda mrefu ambazo zina historia na ushiriki wako ndani yake. Tunapendekeza jibu la aya mbili hadi tatu. Tafadhali thibitisha marejeleo yoyote ya kazi yako mwenyewe kwa viungo pale inapowezekana.
Kwa kawaida unashirikishaje jamii yako uzoefu wako (au mambo uliyojifunza)? Utawezaje kushirikisha kile utakachojifunza katika Wikimania 2026? Mifano ya muhtasari wa kwenye wiki, ripoti, machapisho ya blogu, mazungumzo katika mikutano, n.k., inakaribishwa hapa. Tafadhali jumuisha viungo vya mifano hiyo. Katika jibu lako, tunathamini mpango mahsusi na unaoweza kuthibitishwa wa kushirikisha uzoefu wa Wikimania baada ya Wikimania 2026. Orodha ya nukta (bullet points) yenye maelezo au muktadha kidogo ni muundo unaofaa kwa jibu hili.
Je, wewe ni afisa wa kazi maalum katika miradi ya Wikimedia? Je, unamiliki haki zozote za ziada za mtumiaji kama vile mkabidhi (admin), mkabidhi mkuu (steward), au haki za ukaguzi wa watumiaji (check user rights), au unatekeleza majukumu ya nyuma ya pazia ili kuhakikisha usalama, uendeshaji mzuri, na uendelevu wa miradi ya Wikimedia — kama vile kufanya doria, kujadili makala za ‘Je, unajua?’ na mengineyo? Ikiwa ndivyo, tafadhali eleza. Mwaka uliopita, Wikimania ilizindua kwa mafanikio tukio lake la kwanza kabla ya mkutano kwa watumiaji wenye haki za ziada, ambapo ilitoa ufadhili wa usafiri 50 kusaidia ushiriki na kuhimiza mijadala kuhusu usalama, faragha, na zana. Tunavutiwa kujifunza zaidi kuhusu sifa za waombaji wenye haki za watumiaji zilizoimarishwa. Tafadhali toa mifano ya kazi yako, ukiweka viungo pale inapowezekana.
Ikiwa umetumia zana za AI (akili mnemba) mbali na zile za kutafsiri, kuangalia sarufi, au makosa ya tahajia ili kukamilisha sehemu yoyote ya ombi hili, tafadhali nakili na bandika maswali yote uliyouliza kwa AI hapa chini. Kutozingatia maagizo haya kunaweza kusababisha kufutwa kwa ufadhili wako. Taarifa hizi hazitashirikiwa na wakaguzi. Swali hili halitazingatiwa katika tathmini, kwani linalenga kubaini jinsi tunavyotumia AI na kutuwezesha kuelezea matumizi yake.

Vigezo vya kukataliwa papo kwa hapo

Maombi yatakataliwa katika hatua ya 1 ikiwa chochote kati ya vigezo vifuatavyo visivyofaa vitaonekana:

  1. Mwombaji alipokea ufadhili mwaka 2025 lakini hakukamilisha majukumu yake yaliyotolewa katika Wikimania.
  2. Mwombaji ni mpokeaji wa sasa au wa zamani wa ruzuku yoyote ya WMF na amepatikana kutokufuata Sera ya Ufadhili wa Usafiri wa Wikimedia Foundation.
  3. Mwombaji kwa sasa (amepigwa marufuku duniani kote) na Wikimedia Foundation au jamii yake.
  4. Maombi yasiyokuwa na kitu..
  5. Maombi yanajumuisha maudhui nje ya mada au yenye unyanyasaji.
  6. Mwombaji amekosa kufanya jitihada za kutosha kujibu maswali yaliyo kwenye fomu ya maombi.
  7. Mwombaji amekosa kuonyesha michango au shughuli muhimu yoyote ya Wikimedia ambayo ingeweza kufaa kupewa ufadhili.

Timu Kuu ya Waandaaji (COT) inashirikiana na Wikimedia Foundation na, katika baadhi ya kesi, na vituo vya Wikimedia au washirika wake ili kuamua orodha ya mwisho ya wapokeaji wa ufadhili. Tunahifadhi haki ya kuondoa baadhi ya watu kutokana na mwenendo wao ndani au nje ya wiki. Mifano ni wale walioko kwenye orodha za marufuku za kimataifa na za tukio, walio chini ya adhabu kutoka kwenye Kanuni ya Maadili kwa Wote (UCoC), au wale wanaojulikana kwa COT kama wakiuki wa sheria.

Maombi ambayo hayana vigezo vya kukosa kutimiza yanayohusiana yatafikishwa katika hatua ya 2 kwa tathmini zaidi.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Wikimania 2026 itafanyika wapi?

Wikimania 2026 itafanyika Paris, Ufaransa.

Nani anaweza kuomba?

Je, ufadhili ni kwa washiriki wa mara ya kwanza pekee Wikimania?

Tutapeleka kipaumbele kwa maombi kutoka kwa wale wanaokidhi vigezo vya kutoa mchango mkubwa katika uzoefu wa Wikimania. Tutazingatia jinsi ufadhili utaboreshaje michango ya waombaji kwa dhamira ya harakati baada ya tukio.

Mimi si sehemu ya mshirika. Je, ninaombaje ufadhili?

Watu binafsi wanaweza kutuma ombi bila kujali hali yao ya uanachama wa ushirika.

Mimi ni mfanyakazi wa Wikimedia Foundation. Je, ninaweza kutuma maombi?

  • Sio kama wafanyakazi. Timu Kuu ya Waandaaji (COT) haitoi ufadhili kwa wafanyakazi wa Wikimedia Foundation. Mahudhurio ya wafanyakazi wa Wikimedia Foundation, Kamati za harakati ya Wikimedia, na Wajumbe wa Bodi ya Wikimedia Foundation yanashughulikiwa na shirika lenyewe Wikimedia Foundation.
  • Ikiwa mfanyakazi anayelipwa ataamua kuomba ufadhili, lazima iwe kwa msingi wa kazi yao ya kujitolea. Tunatarajia kwamba wanaweka ni yapi kati ya mafanikio yao yaliyoandaliwa kama mfanyakazi, na yapi yaliyofanywa kwa muda wao wa kujitolea. Tafadhali toa maelezo pale inapohitajika.

Mimi ni mwanachama wa kikundi cha Ufadhili. Je, ninaweza kufanya maombi?

Ndiyo. Wakaguzi wa ufadhili wa kujitolea watakuwa na sifa ya kuomba ufadhili. Ili kuepuka mgongano wa maslahi, maombi yao yataangaliwa na timu inayoundwa na wanachama wa Timu Kuu ya Waandaaji na wakaguzi wa ufadhili wa Wikimania wa awali.

Ikiwa siwezi kuhudhuria Wikimania ana kwa ana, ninawezaje kushiriki?

Kutakuwa na chaguo la kujiunga kwa njia ya mtandao, kwani itakuwa ni tukio la mseto.

Unaweza kuchagua kuandaa tafrija, tukio la kijumuiya lenye shughuli mbalimbali, au kuandaa tukio lako kwa kuzingatia ushiriki katika programu za Wikimania. Hata hivyo, mwaka huu hatutatoa ruzuku kwa matukio yanayohusiana na Wikimania yaliyoandaliwa na washirika kupitia kwenye mfuko wa ruzuku wa Wikimania; ruzuku za matukio hayo zinaweza kuombwa kupitia mchakato wa kawaida wa ruzuku.

Kikomo cha ruzuku ni kipi?

Hakuna kiasi cha dola au thamani maalum. Waombaji watazingatiwa kwa haki bila kujali eneo wanaloishi na umbali au ukaribu wa eneo hilo na tukio.

Mchakato ni upi?

Ombi la ufadhili la Wikimania 2026 litafunguliwa na kuisha lini?

Hatua ya maombi huanza Septamba 10 na kuisha Octoba 31.

Je! ninaweza kutuma maombi ya ufadhili baada ya tarehe ya mwisho?

Hapana. Hii ni kuhakikisha kwamba matokeo ya mwisho ya uamuzi ni yanatolewa kwa wakati na kwa haki kwa waombaji wote. Tunapendekeza uwasilishe maombi angalau siku chache kabla ya tarehe ya mwisho ili kuepuka kukosa.

Je, ninaweza kutuma maombi yangu kwa lugha nyingine tofauti na Kiingereza?

  1. Ndiyo.Wanachama wa kikundi kinachoshughulika na ufadhili watajaribu kadiri ya uwezo wao kupitia maombi.
  2. Ikiwezekana, tunapendelea moja ya lugha nne rasmi za tukio: Kifaransa, Kiingereza, Kihispania, au Kiarabu. Utahitaji kiwango cha kutosha cha Kifaransa au Kiingereza kwa kuhudhulia ana kwa ana na kujitolea katika tukio.

Naweza kuhariri maombi yangu baada ya kuwasilishwa?

Hapana. Fanya ombi lako kwa uangalifu na uhakikishe kuwa unaandika kila kitu unachohitaji kuandika kabla ya kuwasilisha. Tafadhali usitume maombi mara mbili; hii inatengeneza kazi nyingine za ziada kwa wakaguzi.

Mawasilisho ya ufadhili wa Wikimania yatapitiwa lini?

Mawasilisho yatakaguliwa na timu ya ufadhili kwa msingi unaoendelea.

Ufadhili utapitiwa na kutolewa vipi?

Tutaku himiza kutoa jibu linalofaa na kiungo kinacholingana kwenye LimeSurvey. Mara baada ya maombi yote kukamilika na hivyo data zote zitakusanywa, timu inachoshughulika na ufadhili itatathmini kwa pamoja ni nani atakayepokea ufadhili.

Ni lini nitapokea mrejesho wa maombi yangu ya ufadhili?

Majibu yataanza kutolewa Januari. Waombaji wote watajulishwa matokeo yao haraka iwezekanavyo. Hii inaweza kuchukua wiki chache, kwani katika hali fulani watu wengine wanaweza kushindwa kukubaliwa. Waombaji wengine wataelekezwa katika mashirika yao ya ndani ikiwa watachagua chaguo hilo.

Je, waombaji wa ufadhili watajulishwaje kuhusu matokeo?

Tutatumia anwani ya barua pepe uliyoitoa kwenye fomu ya maombi kuwajulisha waombaji. Waombaji wote watawasiliana nasi wakati fulani, bila kujali matokeo. Tunaku himiza kutumia anwani yako ya barua pepe inayotumika au kutoa akaunti yako ya jina la mtumiaji inayotumika kwenye fomu ya maombi.

Ninaweza kupata wapi usaidizi/msaada wakati wa mchakato wa maombi ya Wikimania?

Timu Kuu ya Waandaaji itaandaa mikutano kwa ajili ya kanda mbalimbali na itajibu maswali yatakayowasilishwa kupitia wikimania-scholarships@wikimedia.org na chaneli ya Telegram ya Wikimania. Kwa ujumla, msaada huu utajumuisha:

  1. Maswali ya ufafanuzi kuhusu maombi yaliyowasilishwa
  2. Mambo ya kufanya na yasiyopaswa kufanywa wakati wa kuwasilisha maombi
  3. Changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa kuwasilisha maombi
  4. Hatua zinazofuata baada ya kuwasilisha maombi
  5. Itakuwaje nisipopata ufadhili

Maswali ya Ustahiki

Je, ufadhili ni kwa ajili ya washiriki wa mara ya kwanza pekee wa Wikimania?

Tutatoa kipaumbele kwa waombaji wanaokidhi vyema vigezo vya kuchangia katika uzoefu wa Wikimania. Pia tutazingatia jinsi ufadhili huo utakavyoboresha mchango wa waombaji katika kutekeleza malengo ya Wikimedia baada ya tukio.

Mimi si sehemu ya mshirika. Je, ninaombaje ufadhili?

Watu binafsi wanaweza kutuma maombi bila kujali hali yao ya uanachama wa ushirika.

Ikiwa siwezi kuhudhuria Wikimania ana kwa ana, ninawezaje kushiriki?

Kutakuwa na fursa ya kushiriki kwa njia ya mtandao kwani tukio hili litakuwa na muundo wa mseto (hybrid). Unaweza kuchagua tafrija (watch party), tukio lenye shughuli mbalimbali, au kupanga tukio lako kulingana na programu za Wikimania. Hata hivyo, mwaka huu hatutatoa ufadhili kwa matukio yanayohusiana na Wikimania yanayoandaliwa na washirika kupitia mfuko wa ruzuku wa Wikimania; aidha ruzuku za mikutano hiyo zinaweza kuombwa kupitia mchakato wa kawaida wa ruzuku.

Kikomo cha ruzuku ni kipi?

Hakuna kiasi cha dola au thamani maalum. Waombaji watazingatiwa kwa haki bila kujali eneo wanaloishi na umbali au ukaribu wa eneo hilo na tukio.

Nimepata/sijapata ufadhili, na...

Je, ni mahitaji gani ya utoaji wa ripoti?

Badala ya kuandika ripoti, tunawaomba wanufaika wa ufadhili kusaidia kwa kujitolea kwenye tukio kwa muda wa saa 4 hadi 6. Tutashirikiana nawe kutafuta jukumu linaloendana na mahitaji, ujuzi, na uzoefu wako. Hata hivyo, unaweza pia kuandika ripoti au chapisho kwenye Diff ikiwa utapenda!!

Ninaweza kumpa ufadhili wangu mtu mwengine?

Hapana. Ili kuwepo na usawa, ufadhili ulipitiwa na kutolewa kwa mpangilio fulani wa sifa. Ikiwa mpokeaji atathibitisha kukataa, utawasilishwa kwa mtu mwingine kwa utaratibu wa ukaguzi kama ilivyo kawaida.

Iwapo nitakataa ufadhili wa mwaka huu, naweza kuutumia kwa Wikimania ya mwaka ujao?

Hapana. Kila mwaka Wikimania huandaliwa chini ya kaulimbiu tofauti kulingana na maamuzi ya Timu Kuu ya Waandaaji wa mwaka husika katika maeneo mbalimbali. Tutakuhimiza uombe tena kwa mwaka unaofuata, na tutahakikisha tunazingatia mchango wako endelevu na wenye thamani katika mchakato wetu wa mapitio.

Ikiwa sikupokea ufadhili, naweza kuomba timu ya wafadhili kukagua ombi langu tena?

Hapana. Mchakato wetu wa ukaguzi unahusisha hatua kadhaa za uangalifu, na kwa masikitiko, unaweza kukamilishwa mara moja pekee.

Niliomba ufadhili lakini sikupata. Nifanye nini sasa?

Kupata ufadhili si sharti ili kushiriki Wikimania; unaweza pia kujisajili na kushiriki mradi tu uweze kugharamia mwenyewe matumizi yako.

Kama huwezi kugharamia gharama zako mwenyewe, tunakuhimiza kuwasiliana na shirika la eneo lako. Wanaweza kuwa na programu yao ya ufadhili au kuandaa tukio katika eneo ulilopo!

Niwasiliane na nani kwa taarifa zaidi?

Unaweza kuwasilisha maswali yako kwa wikimania-scholarships@wikimedia.org.

Ufadhili wa matukio yanayohusiana na washirika

(Katika miaka iliyopita, hii iliitwa matukio ya satellite) Washirika wa Wikimedia wanaweza kutumia fedha zilizopatikana kupitia Mfuko wa Jumla wa Ruzuku wa Wikimedia Foundation (GSF) kuandaa tukio linalohusiana na Wikimania katika eneo lao, hata kama tukio hilo halikuorodheshwa awali katika maombi yao ya GSF. Waliopewa ruzuku ya GSF wanaweza kubajeti fedha ndani ya bajeti yao kadri inavyohitajika, na, kwa mujibu wa makubaliano ya Mfuko wa Jumla wa Ruzuku, Foundation inaomba tu kwamba Maafisa wa Programu wajulishwe iwapo tofauti hiyo ni zaidi ya 20% kutoka katika bajeti yao ya awali.

Tunawahimiza washirika wote wanaopenda kuandaa tukio linalohusiana na Wikimania kuandika taarifa za tukio lao kwenye Matukio yanayohusiana na washirika, ili washirika waweze kuratibu kati yao, kuhimiza ushirikiano na uhusiano kati ya Wanawikimedia, na pia kufanya matukio yao kwa ufanisi zaidi.

  • Washirika wanaotaka kufanya matukio mubashara (live stream) kwenye Wikimania wanapaswa kuwasiliana na timu ya programu kupitia wikimania@wikimedia.org mara tu wanapokuwa na taarifa za tukio lao.
  • Timu Kuu ya Waandaaji itatoa msaada wa kiufundi kwa makundi/washirika wanaotaka kurusha matukio mubashara (livestream) kuelekea Wikimania.
  • Tafadhali tumia Matukio yanayohusiana na washirika kujadili mawazo.

Nina maswali zaidi na hayapo kwenye Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)

Unaweza kuwasiliana na kamati wakati wowote kupitia wikimania-scholarships@wikimedia.org. Tutakuwa tukifanya vikao vya wazi kwa kila mtu anayevutiwa na Wikimania ili kuja na kuuliza maswali kuhusu: Programu, Ufadhili, Masuala ya Logistic, Hafla za Wikimania, na jinsi ya kushiriki katika Wikimania. Hayo yote yatapatikana hivi karibuni.

Angalia taarifa ya faragha ya dodoso.