Jump to content

2023:Taarifa

From Wikimania
This page is a translated version of the page 2023:Updates and the translation is 97% complete.
Outdated translations are marked like this.


Angalia sehemu hii kwa taarifa za mara kwa mara kama Timu Maalumu ya Uratibu (COT) na Kamati ya Uongozi (SC)kwa maendelea na upangaji wa Wikimania 2023.Kwa taarifa nyingine muhimu, tembelea diff post.

Taarifa

Septemba 20 2022

 • Wito kwa watu wa kujitolea umekamilika kwa Awamu ya 1. Shukrani kwa wote ambao wamejisajili! Kutakuwa na fursa za ziada za kujitolea, kwani tutahitaji usaidizi zaidi kadri Wikimania inavyokaribia. Unaweza kutembelea 2023:Watu wa kujitolea ili kujua zaidi.

Timu Maalumu ya Uratibu ya Wikimania 2023 na ESEAP asante kwa ushirikiano wako, na bado kutakuwa na fursa zaidi ikiwa haujajiandikisha bado.

Kinachotokea baadaye: Timu Maalumu ya Uratibu (COT) itachunguza mapendekezo ya maeneo ambayo watu wa kujitolea wameonyesha. Baadhi ya majukumu ya papo hapo yatataka mtu kupitia ukaguzi wa Wikimedia Foundation m:Special:MyLanguage/Trust & SafetydidiTrust & Safety kama kusaini makubaliano ya siri (NDA) kwa sababu ya kupata habari binafsi. Baada ya kukamilika, tutatuma mialiko ya kujiunga na kamati ndogo.

Usikate tamaa, awamu hii itachukua muda kidogo, na lengo letu litakuwa katika maeneo ambayo COT inahitaji kuanza mapema, kama timu za udhamini. Kama tukio la mseto, Wikimania itaunganisha matukio mawili (ana kwa ana na mtandaoni) kwa hivyo kutakuwa na fursa nyingi zinazokuja.

COT inapoanza majaribio ya chaguzi, tutakuomba pia ushiriki katika majadiliano hayo, kwa kutumia zana mbalimbali zitakazopatikana.

Iwapo umekosa awamu hii, bado kuna awamu zinaendelea kwa watu wa kujitolea. Tafadhali tembelea kwenye ukurasa wa kujitolea kwenye 2023:Watu wa kujitolea kwa maelezo zaidi.

Septemba 12 2022

Wito wa kujitolea umewekwa kwenye chaneli nyingi - Wikimedia-L, vikundi vya Telegraph, vikundi vya Facebook, kwenye wiki. Tarehe ya mwisho 19 Septemba 2022.

Septemba 5 2022

 • Wito wa Timu Maalumu ya Uratibu ya 2023 umefungwa huku wanachama wapya wa timu wakiarifiwa

Septemba 1 2022

 • COT, Kamati ya Usimamizi, WMF wakijadiliana
  • ujumuishaji wa IRL, Mtandao, Muundo wa matukio ya Satelaiti
  • Machaguzi ya ukumbi
  • ratiba ya maandalizi kwa ajili ya mawasilisho ya programu, udhamini, na matukio satelaiti
 • Wikimania.wikimedia.org kuomba tiketi ya Phabricator kuwa tayari kwa 2023
 • COT & SC wanachunguza kwa kina zaidi athari za vipengele, shughuli na muundo wa Wikimania

Agosti 26 2022

 • Mji: Singapore - imethibitishwa
 • Tarehe: Julai/Agosti
 • COT: inaendelea kukua tazama hapo juu wito
 • Dhima: "Nguvu ya ushirikiano mbalimbali: Kushiriki maarifa huleta watu pamoja" – dhima ya awali mwaka 2020


Mpangilio wa tukio